Jembe FM@jembefm

93.7 Mwanza
PAMOJA SANA:
SIKILIZA LIVE-JEMBE FM HAPA
👇

www.jembenijembe.com/

2,346 posts 17,838 followers 62 following

Jembe FM

Je ni kweli Ali Kiba kafanya mabadiliko kwenye mkataba wake na Costal Union?
Mkataba utakao mfanya aamue kucheza mechi flani au asicheze... Klabu imeweka wazi kuhusu hilo kupitia Sport Report ya Jembe Fm usikose kusikiliza kwanzia saa 3usiku.


4

Jembe FM

TUPE UTABIRI WAKO LEO KATIKA #UCL.
.
.
Usiku wa Leo pale Barani Ulaya kunapigwa mechi za mwisho za kundi A, B, C, na D kwenye michuano ya Uefa champions League.
Katika kundi B kuna mechi kati ya Barcelona na Tottenham mchezo utakaopigwa pale Camp Nou na mechi ya Inter Milan na Psv mchezo utakaopigwa pale Giuseppe Meazza michezo yote ikipigwa kwanzia saa 5 usiku.
Inter na Tottenham kila timu inapoint 7 katika hili kundi Tottenham kila timu hapo inahitaji point huku kila timu hapo inamuombea mwenzake kipigo.
Tupe utabiri wako nani ataenda hatua ya 16 bora hapo?
Utabiri wako utawekwa hadharani kwenye Kipindi cha Sport Report, Jembe Fm kwanzia saa 3:00 usiku.


37

Jembe FM

Hayawi hayawi sasa yamekuwa Mzigo mpya kutoka #FemaRadioShow @feminahip umetua mikononi mwa wana Kanda ya Ziwa na safari hii tutasikika moja kwa moja kupitia @jembefm 93.7 msimu unalenga namna ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi mkoa wa Mwanza. Unadhani nini sababu ya Vifo vya uzazi mkoa Mwanza? Maoni yako tutayapitia hapa !!! ni Ijumaaa hii tarehe 14 Dec 2018 kuanzia saa 3:00 Usiku ,Tusikilize popote duniani kupitia #tuneIn93.7 pia tufatilie kupitia page zetu @jembefm @feminahip twitter feminahip fb feminahip na instagram @feminahip #MsimuMpyaVifovyaUzaziSasaBasiMkoaMwanza


3

Jembe FM

Ufafanuzi kutoka Idara ya Uhamiaji kuhusu taarifa ya ubadilishwaji wa utaratibu wa kutoa viza, kwa raia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Angola.


1

Jembe FM

Rais Magufuli ameiagiza TRA na Wizara ya Fedha kutoza kodi ya nyumba ya TZS 10,000 kwa nyumba za kawaida, TZS 20,000 kwa nyumba za ghorofa zilizopo wilayani na vijijini na 50,000 kwa nyumba kubwa. Na utozaji huo uzingatie hati ya kiwanja na sio idadi ya nyumba kwenye kiwanja.


3

Jembe FM

Desemba 9 miaka 57 ya Uhuru wetu, tunawaahidi kuendelea kufanyakazi bila kuchoka katika kuwatumikia watanzania. Uhuru wetu ni amani yetu na ndio maendeleo yetu-


2

Jembe FM

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametoka msamaha kwa wafungwa 4,477 nchii,

Rais Magufuli ametoa msamaha huo ktk kuelekea sherehe za Uhuru,. .
.

Rais Magufuli amesema msamaha huu utawahusu wazee kuaniza miaka 70 na zaidi wafungwa wagonjwa, wafungwa wa kike walioingia gerezani wakiwa wajawazito na walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya pamoja na wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili ikiwa ni pamoja na wafungwa waliotumikia robo ya adhabu zao wapunguziwe adhabu zao na ameongeza kuwa msahama huu hautawahusu wafungwa wanaotumikia baadhi ya adhabu zikiwemo kunyongwa,kifungo cha maisha,biashara ya dawa za kulevya, biashara za binadamu, makosa ya unyanganyi, kukutwa na viungo vya binadamu, makosa ya kupatikana na siraha kama risasi, makosa ya shambulio LA aibu kama vile kunajisi, kulawiti, kubaka, kuwapa mimba wanafunzi wa shule za msingi na secondary, uhujumu uchumi, rushwa, ujangiri na walioingia gerezani baada ya tarehe moja mwezi desemba mwaka huu.


2

Jembe FM

JESHI la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia Simon Saulo Ngatunga 38 aliyekuwa Mkurungenzi wa Utumishi katika Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi – Sikonge, Tabora, na mfanyabiashara mmoja kwa tuhuma za utapeli.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Girres Muroto wakati akizungumza na wanahabri jijini humo.

Tumemkamata mtu mmoja anaitwa Hassan Katundu (29) mfanyabiashara na mkazi wa Yombo-Buza jijini Dar es Salaam, alikuwa akijifanya ofisa usalama wa taifa, na kuwatapeli wananchi akiwalaghai wampatie pesa ili awatafutie nafasi za kazi. Baada ya kutimuliwa kazi, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi Ofisi ya Rais Tamisemi Sikonge, Simon Ngatunga, amekuwa akimtumia huyu ofisa feki wa usalama wa taifa kumtafutia ajira, hivyo wote tumewatia mbaroni na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani. -


0

Jembe FM

WANAFUNZI WATATU WAANGUKIWA NA UKUTA.
.
.
Wanafunzi watatu wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa jengo la moja ya madarasa ya shule ya Msingi Bwawani ambapo katika hao waliojeruhiwa wengine ni wanafunzi wa shule ya Msingi Kijichi.
Ajali hiyo ya kuanguka kwa ukuta imetokea katika Shule ya Msingi ya Kijichi ambapo wanafunzi 3 waliojeruhiwa wamelazwa hospitali ya Temeke kwa ajili ya matibabu
-
RPC wa Temeke, Andrew Masatya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo . -


0

Jembe FM

Waziri wa Afya, Ummy mwalimu amezitaka hospitali na vituo vyote vya serikali kufunga mashine za utambuzi wa alama za vidole (biometric) ndani ya siku 60, ili kudhibiti mahudhurio ya wafanyakazi.


10

Jembe FM

HATMA YA MWANAMKE ALIYETAKA KUGOMBEA URAISI RWANDA KUJULIKANA LEO. .
Mahakama mjini Kigali leo inatarajia kutoa uamuzi wake wa mwisho kuhusu kesi dhidi ya mwanasiasa wa upinzani bi Diane Rwigara na mamake Adeline Rwigara.
Wawili hao wameshitakiwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka.
Muendasha mashtaka ameshaomba mahakama kuwapa kifungo cha miaka 22 jela.
Walikanusha madai hayo wakisema yana misingi ya kisiasa. Marekani imeishinikiza Rwanda kuondoa mashitaka hayo,lakini Rwanda imejibu kwamba haishinikizwi na yeyote na kuomba vyombo vya sheria visiingiliwe.
#chanzobbcswahili


1

Jembe FM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Desemba 5, 2018, amemtembelea na kumjulia hali Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Kumjulia hali, Rais Dkt. John Magufuli ameshiriki dua ya kumuombea Afya Njema iliyoongozwa na familia ya Rais huyo mstaafu.


0